Star Tv

Rais wa Marekani Joe Biden amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin hafai kuendelea kubaki madarakani baada ya uvamizi wa Uruai nchini Ukraine.

Katika hotuba yake nchini Poland Rais wa Marekani Joe Biden pia alionya kwamba hatua kali zitachukuliwa iwapo vikosi vya Urusi vitaingia japo kwa inchi moja tu katika eneo la nchi yoyote mwanachama wa muungano wa kijeshi wa NATO. Rais huyo wa Marekani ameyasema hayo mwishoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Poland siku ya Jumamosi.

Hata hivyo ikulu ya Marekani mara moja ilieleza kuwa hotuba hiyo kali isiyo ya kawaida ya Rais Biden haikumaanisha kuwa Marekani inataka mabadiliko ya utawala nchini Urusi na kufafanua zaidi kwamba hoja ya Rais Biden ilimaanisha kuwa Putin hawezi kuruhusiwa kutumia mamlaka yake juu ya majirani zake au eneo lolote la nchi wanachama wa NATO. Afisa huyo ikulu alisisitiza kuwa Biden hakuwa akijadili mamlaka ya Putin nchini Urusi, au mabadiliko ya utawala.

Awali ya yote, Rais Joe Biden alifanya mazungumzo na Rais wa Poland Andrzej Duda mjini Warsaw na alimuhakikishia kwamba Marekani imejitolea katika maswala ya ulinzi wa eneo la Ulaya Mashariki. Vile vile Biden alisisitiza kwamba mkataba wa ulinzi wa nchi zote wanachama wa jumuiya ya NATO ulikuwa "dhamira njema."

Wakati wa hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni ya Poland, Biden alisema amevutiwa mno na ukarimu wa watu wa Poland kwa jinsi walivyofungua mioyo na nyumba zao na kuwasaidia wakimbizi wa Ukraine. Alisema kama mwanachama mkubwa Zaidi wa NATO katika kambi ya zamani ya mashariki, Poland ina jukumu muhimu katika jibu la Magharibi kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Poland imewachukua wakimbizi wa Ukraine zaidi ya milioni 2.2 kati ya jumla ya wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni 3.5 walioikimbia Ukraine tangu uvamizi wa Urusi uanze nchini humo zaidi ya mwezi mmoja uliopita.

Rais huyo wa Marekani alibainisha kuwa licha Poland kuchukua jukumu kubwa, lakini jukumu hilko inapaswa kuwa la NATO. Warsaw imetoa mwito kupelekwa wanajeshi wa kulinda amani wa NATO nchini Ukraine, lakini Marekani imelikataa wazo hilo.

#ChanzoDWKiswahili

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.