Star Tv
ais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika - ambayo hupewa viongozi wa Afrika ambao wameonekana kuwa na utawala mzuri. Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia. Wakati aliposhinda uchaguzi wa Rais nchini humo mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kadhaa na tuzo hiyo ya amani ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kusaidia kuiimarisha nchi hiyo.Mjasiriamali Mwingereza mwenye asili ya Sudan Mo Ibrahim alianzisha tuzo hiyo mwaka 2007 kwa ajili ya kuwatunukia viongozi walionesha kazi nzuri wakati wa kipindi cha uongozi wao ndani ya bara la Afrika, amballo madikteta na watawala wadhalimu wamerudisha nyuma maendeleo ya bara hili. Tuzo hii ambayo inapaswa kutolewa kila mwaka , kwa mara sita mfululizo ilishindwa kupata mtu, kutokana na viongozi kukosa sifa za kushinda tuzo hiyo. Ellen Johnson Sirleaf atapata dola za Kimarekani milioni tano zitakazogawanywa kwa miaka kumi, na dola laki mbili kwa maisha yake yote. Add a comment
Kiongozi wa Chama tawala nchini Afrika kusini cha ANC Cyril Ramaphosa amethibitisha kuwa chama kitafanya uamuzi wa mwisho juu ya hatma ya Rais Jacob Zuma. Add a comment
Takriban miaka mitano baada ya kujitoa katika jumuiya ya madola leo Gambia inajiunga upya. Add a comment
Rais mpya wa Liberia George Opong Weah amemfuta kazi Waziri wa sheria Charles Gibson, baada ya malalamiko ambayo yamesababisha kupokonywa leseni ya Uwakili baada ya kumtapeli mteja wake. Kabla ya uteuzi wake, Gibson alikuwa amepatikana na hatia hiyo na Mahakama ya Juu baada ya kumtapeli mteja wake Dola za Marekani 25,000 na kuagizwa kuzirejesha. Rais Weah amemteua Musa Dean aliyekuwa Wakili katika Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi hiyo. Mwanasoka huyo wa zamani wa Liberia alichaguliwa kuwa rais mteule ikiwa ni katika jaribio lake la pili. Add a comment
Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU. Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani. Add a comment

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.