Star Tv

Katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayohimiza uchumi wa viwanda, jeshi la Polisi nchini limetakiwa kuwahimiza askari wake kujikita katika masuala ya ujasiriamali ili kuyafikia maendeleo yanayotokana na biashara kwa kupatiwa mafunzo na elimu ya ujasiramali.

Ujasiriamali na biashara ni jambo linalohimizwa kwa kila mtanzania mwenye utimamu wa akili, na lengo kuu likiwa ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na hata Taifa kwa ujumla- ambapo jeshi la Polisi - askari wake wametakiwa kutojiweka kando na badala yake wachangamkie fursa za kibiashara.

Julius Mjengi ni kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa , naye anaona suala ujasiriamali ndiyo wimbo unaopaswa kuimbwa kwa pamoja kwa kila mtanzania wa Taifa hili.

Rai hii imetolewa katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya mtandao wa Polisi wa kike mkoani Iringa, shughuli ambayo Rita Kabati mbunge wa Viti maalumu CCM mkoani Iringa ndiye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hii.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.