Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Zitto Kabwe amefanya ziara katika Ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam nchini (LHRC), Ofisi za Foundation for Civil Society (FCS) pamoja na Legal Services Facility (LSF).
Zitto anafanya ziara hiyo kwa lengo la ziara husika ni Uongozi Mpya wa TCD kujitambulisha kwa wakuu wa taasisi hizo pamoja na kuona namna nzuri ya TCD kushirikiana na LHRC, FCS pamoja na LSF katika jitihada za kuwezesha TCD kufanya kazi vizuri kufufua demokrasia na kutoa nafasi ya mijadala kati ya vyama vya siasa, serikali na Asasi za kiraia.
Katika ziara hiyo ambayo Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa TCD aliambatana na Afisa wa TCD, ndugu Lucy Agostino ilianza siku ya Agosti 28, Jumamosi kwa kutembelea chama mwanzilishi wa TCD, Chadema, na anatarajia kutembelea na kufanya mazungumzo na vyama vingine wanachama wa TCD ambao ni NCCR Mageuzi, CUF na CCM.
Aidha, Zitto anatarajia pia kutembelea na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi za Dini, Mabalozi, Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na wadau wengine wa demokrasia siku zijazo.