Mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kwamba corona inaweza kuisha mwishoni mwa mwaka huu iwapo nchi zote duniani zitachukua hatua kabambe za kukabiliana na maambukizi.
Kiongozi huyo wa WHO alilkuwa akizungumza katika kikao cha 150 cha shirika hilo la afya duniani cha kamati kuu kilichofanyika mjini Geneva.
Akizungumza katika mkutano huo, Tedros amesema kuwa WHO inashirikiana katika ngazi za kikanda, kitaifa na kimataifa katika juhudi za kuutokomeza ugonjwa wa Covid.
Aidha amesema kwamba shirika hilo limekuwa likitoa raslimali, mikakati, na ujuzi wa kiufundi unaohitajika katika kudhibiti corona kwa nchi husika.
#ChanzoBBC