Mamia ya watu wamejitoalea kuvua nguo zao na kubaki watupu ili wachorwe picha zinazoelezea namna Bahari ya kifo au 'Dead Sea' inavyoendelea kunyauuka.
Watu hao wake kwa waume wapatao 300, walikuwa wamevaa nguo za ndani nyeupe na hivyo kuacha sehemu nyingine za mwili wao wazi ili kutoa fursa kwa mpiga picha Mmarekani Spencer Tunick, ambaye amefanya sanaa hiyo katika maeneo mengine ya fukwe za bahari duniani kama njia ya kuhamasisha watu kutunza bahari.
Mpiga picha huyo amewahi kuendesha kampeni hiyo katika maeneo kama eneo la barafu la Uswiss na ufukwe wa Afrika Kusini.
“Matembezi yangu nchini Israeli yamenipa uzoefu wa kipekee na ninafurahi wakati wote kurejea hapa na kupiga picha katika nchi pekee ya Mashariki ya Kati inayoruhusu sanaa ya aina hii,”- Alisema Tunick.
Aidha inaelezwa kuwa upigaji picha huo ulihamasishwa na Wizara ya utalii ya Israeli.