Star Tv

Wanamgambo wa kundi la Kiislamu la Boko Haram wametoa video mpya ambayo inasema wapiganaji wake wa Boko Haram ndio waliotekeleza mauaji ya wakulima 78 katika eneo la Zabarmari karibu na Maiduguri kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Jumamosi, wanaume waliokuwa na silaha waliotumia pikipiki na kutekeleza shambulizi la kinyama dhidi ya wakulima wa mashamba ya mpunga.

Wakati huohuo, wabunge wa Nigeria wamefanya mazungumzo na rais Muhammadu Buhari juu ya mauaji hayo na Wabunge hao wamesema suala hilo ni la kupewa umuhimu mkubwa.

Katika video iliyoonekana na BBC, Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram–aliyefunika uso wake, alisema kundi hilo lilitekeleza shambulizi dhidi ya wakulima wa mashamba ya mpunga wikendi iliyopita.

Hilo linawadia wakati raia wa Nigeria wanaendelea kughadhabishwa na mauaji hayo wanayoyaelezea kama mabaya zaidi kutokea katika miezi ya hivi karibuni.

Aidha, Umoja wa Mataifa umefuta idadi ya waliojeruhiwa ya watu 110 iliyokuwa imetoa awali, na kusema kuwa idadi kamili ya walioathirika bado haijulikani.

Jeshi limekosolewa pakubwa kufuatia mauaji hayo lakini limelaumu ukosefu wa vifaa stahiki kuweza kukabiliana na kundi hilo. Pia limeshutumu wakaazi kwa kushirikiana na wanamgambo hao katika kuwapa taarifa.

 

Latest News

BIDEN KUSAINI MAAGIZO 12 YA RAIS.
17 Jan 2021 07:08 - Grace Melleor

Rais mteule wa Marekani Joe Biden atatia saini maagizo 12 ya rais siku ya kuapishwa kwake kuwa rais wiki ijayo ili kushu [ ... ]

MUSEVENI AWAONYA WAFUASI WA UPINZANI KUTOZUA GHASIA.
17 Jan 2021 06:10 - Grace Melleor

Rais wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni jana Jumamosi ameonya kuwa vikosi vya usalama vitatumia nguvu kuzima ju [ ... ]

WATU WAWILI WANUSURIKA KUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
17 Jan 2021 05:42 - Grace Melleor

Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Musoma mkoani Mara wamenusurika kuawa na wananchi wenye hasira kali kutoka kwa vijana  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.