Wizara ya Afya nchini China imeripoti uwepo wa visa vipya 17 vya Corona, Visa hivyo ni kutoka miji ya Wuhan na Jilin.
Mji wa Jilin umewekwa katika zuio la kutotoka nje baada ya visa 10 katika visa hivyo 17 ambavyo vimeripotiwa kutokea ndani ya mji huo na mamlaka bado hazijatangaza kuwa mji huo utakuwa kwenye katazo hilo mpaka lini.
Hofu inatanda miongoni mwa watu wakihofia kuwa yawezekana ugonjwa huu ukarudi tena kama endapo hatua stahiki hazitachukuliwa za kudhibiti maambukizi mapya yasiendelee kutokea.
Mpaka sasa China ina jumla ya visa 82,918.780 vya ugonjwa huo, wagonjwa 78,144 wameripotiwa kupona na vifo vilivyotokea ni 4600.