Star Tv

Serikali imeamua kuanza kutekeleza miradi ya maji nchini kupitia mamlaka za maji za mikoa baada ya miradi hiyo iliyokuwa ikijengwa na makandarasi kuchukua muda mrefu bila kukamilika.

Waziri wa maji  profesa Makame Mbarawa ametangaza uamzi huo wakati akiikabidhi MWAUSWA mradi wa maji ulioko kata ya Kikubiji katika wilaya ya Kwimba jijini Mwanza uliotumia miaka sita bila kukamilika.
Ameeleza kuwa matatizo ya maji katika maeneo mengi nchini yamesababishwa na baadhi ya makandarasi na wataalamu wasio waadilifu. Baada ya kukabidhiwa mradi huo mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira jijini mwanza MWAUWASA mhandis Anthon Sanga ameahidi kuwa mamlaka yake itajitahidi kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika ndani ya siku sitini. Awali akitoa taarifa ya mradi huo mhandisi wa maji wilayani kwimba Boaz Pius amesema kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza tangu mwaka 2013 na ikiwa utakamilika baada ya kukabidhiwa MWAUWASA unatarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi elfu kumi na sita.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.