Watu wenye silaha wamevamia hospitali mbili katika mashambulizi tofauti kaskazini-magharibi na zilizopo katikati mwa Nigeria.
Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) wamesema watu wenye silaha walishambulia kituo cha afya katika kata ya Birnin Magaji katika wilaya ya Gummi kwenye jimbo la Zamfara siku ya Jumatatu, na kumteka nyara mtu mmoja.
MSF kupitia ukurasa wake wa twitter imebainisha kwamba kundi lililojihami kwa silaha lilivamia kituo cha afya na kumteka nyara mzee mmoja mfanyakazi wa uuguzi na baadaye waliharibu dawa na chakula cha matibabu.
Madaktari hao kutoka shirika la misaada linasaidia kuendesha sehemu ya kituo kinachosaidia watoto wenye utapiamlo nchini humo.