Umoja wa Mataifa umezitaka mamlaka nchini Libya kuagiza uchunguzi "haraka, huru na wa uwazi" kuhusu mauaji ya wahamiaji 15 karibu na mji wa pwani wa Sabratha.
Miili hiyo ilipatikana siku ya Ijumaa, baadhi ikiwa imechomeka ndani ya boti iliyoungua.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema mauaji hayo yanakisiwa kusababishwa na mapigano kati ya magenge hasimu ya wasafirishaji haramu wa binadamu na inataka wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Aidha kwa muda mrefu Libya imekuwa njia kuu ya usafirishaji wa wahamiaji kwenda Ulaya.
#ChanzoBBC