Serikali ya Tanzania inatekeleza miradi ya Maendeleo chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia katika baadhi ya halmashauri zake hapa nchini ambapo baadhi ni pamoja na miradi ya ujenzi wa barabara, maji na ile ya sekta ya Afya.

Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa ni miongoni mwa wanufaika wa miradi hiyo na serikali imeiagiza kuhakikisha inatafuta eneo lingine la kujenga kituo cha kuegesha Malori linalokidhi vigezo na mahitaji badala ya eneo lililojengwa kituo kipya cha Malori liliopo eneo la Utengule ambalo linaonekana kuwa ni dogo hata kabla ya mradi huo kuzinduliwa.

Kituo cha Malori cha Utengule kilichopo kwenye barabara ya Sumbawanga –Tunduma katika Manispaa ya Sumbawanga kimejengwa chini yaufadhili wa miradi ya maeneleo ya Benki ya Dunia ambayo inatekelezwa kwenye halmashauri 18 hapa nchini na kituo hili kimegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 na kimeonekana kuwa ni kidogo kutokana na uwezo wake wa kupokea sio chini ya malori 45 hadi 50 kwa wakati mmoja,na kimeelezwa kuwa hakilingani na mahitaji ya ukuaji wa mji wa Sumbawanga dhidi ya malori yanayoingia hivi sasa na miaka kadhaa ijayo.

Picha na mtandao.

Latest News

Diamond ahojiwa na Polisi kuhusu picha za mitandaoni
17 Apr 2018 12:43 - Joseph Musyoka

Mwanamziki maarufu wa Bongo fleva Nasibu Abdul Juma maarufu Diamond Platnumz amekuwa akihojiwa na Polisi kuhusu video il [ ... ]

Mwanasiasa wa Kenya Kenneth Matiba amefariki
16 Apr 2018 11:22 - RobinLeah Madaha

Mwanasiasa shupavu wa upinzani nchini Kenya Kenneth Stanley Njindo Matiba amefariki.

Mshairi kufungwa jela kwa kuhamasisha umoja Somalia
16 Apr 2018 09:23 - RobinLeah Madaha

Mahakama ya serikali iliyojitenga ya Somaliland imemfunga jela miaka mitatu ,msichana anayeimba mashairi kwa kosa la kuh [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2018 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.