Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) cha kuongeza ubeti katika wimbo wa taifa ambao waliimba katika kikao cha kumchagua mwanachama atakayepeperusha kijiti cha kuwania urais kupitia chama hicho.
Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari na kusema kuwa kitendo hicho si cha busara kwa kuwa wimbo huo si wa chama chochote ni wa taifa hivyo unapaswa kutumiwa vyema na kuheshimiwa na watu wote pale unapoimbwa katika matukio mbalimbali.
Aidha, mbali na hilo Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi Agosti 15, 2020 watazindua nyimbo zote ambazo nitatumia katika Kampeni mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru na amesema wasanii wote wa Bara na Visiwani mbalimbali watahudhuria haflahiyoi akiwemo Diamond, Harmonize watakuwepo.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bwana Polepole amesema mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama hicho atachukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi hiyo wiki hii jijini Dodoma ambapo amesisitiza kuwa siku ya kiongozi huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kuchukua fomu itatangazwa.