Star Tv

Viongozi mbalimbali kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Julai 14, wamejitokeza kuchukua fomu za kupata ridhaa ya kuteuliwa kuwa wagombea katika majimbo mbalimbali nchini.

Baadhi ya viongozi hao ni aliyekuwa mbunge wa zamani wa jimbo la Siha, na mkuu wa mkoa mstaafu wa Tabora Aggrey amechukua fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Siha, Na amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya ya Siha Mwanaidi Mbisha katika Ofisi za CCM Wilaya, Na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, amechukua fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Arusha Mjini, ambapo amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa CCM Wilaya ya Same Victoria Mahembe.

Mbali na viongozi hao waliowahi kuwa wakuu wa mikoa Pia baadhi ya mawaziri wamechukua fomu leo akiwemo; Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo Achukua Fomu Ya Kugombea Ubunge Jimbo la Kisarawe amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kimteue kwa ajili ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kisarawe.

Baadhi ya waliokuwa Mawaziri wa sekta tofauti nao hawakusita kuchukua fomu za kuomba ridhaa ambao; ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ambaye amechukua ya kugombea Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe, Waziri wa Uwekezaji, Angellah Jasmine Kairuki amechukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Same Magharibi.

Pia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako naye amechukua fomu ya kuomba ridhaa chama chake ili kiweze kumteua, aweze kugombea Ubunge katika jimbo la Kasulu Mjini, Pia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Dkt.Angelina Mabula amechukua fomu ya kutetea kiti chake cha ubunge katika ofisi ya Chama cha CCM wilaya ya Ilemela.

Naibu Spika wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye hakubaki nyuma ambapo mumewe James Andelile Mwainyekule alimsindikiza mkewe Dkt.Tulia Ackson ambaye amemaliza muda wake pia amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini kupitia tiketi ya CCM.

Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aitwaye Fredrick Lowassa  naye amechukua fomu ya kugombea ubunge Monduli, mkoani Arusha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na amekabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa chama hicho Wilaya ya Monduli, Langael Akyoo.

Aidha kwa upande wa Chama cha upinzani ambapo tayari wabunge mbalimbali wamepigiwa kura za maoni kuomba ridha ya kuteuliwa kugombea ubunge, Mbunge wa Arusha Mjini aliyemaliza muda wake, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa twitter amesema sheria ingeruhusu, angetaka wagombea wote wa CCM Arusha ashindane nao.

“Nime sikia sikia majina ya wagombea Ubunge Arusha Mjini kupitia ccm.Kama sheria ingeruhusu wote 30 kushindana nami na picha zao wote kutokea kwenye karatasi ya kura dhidi yangu,bado wangeimba wimbo walio imba 2010/2015.Twendeni mpaka mwanzo wa bahari,wepesi sana hawa.” -Ameandika Godbless Lema.

Leo Jukai 14, Chama Cha Mapinduzi kimefungua pazia kwa wanachama wake kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo,  ambapo zoezi hilo linatarajiwa kusitishwa tarehe 17 Julai 2020.

Latest News

WANASHERIA WA BOBI WINE WARUHUSIWA KUMUONA MTEJA WAO.
22 Jan 2021 08:40 - Grace Melleor

Jeshi la UPDF na polisi nchini Uganda wamewaruhusu wanasheria wa waliokuwa wa mgombea wa kiti cha urais Robert Kyagulany [ ... ]

UINGEREZA YAPIGA MARUFUKU ABIRIA KUTOKA TANZANIA, DRC.
22 Jan 2021 08:18 - Grace Melleor

Abiria wote kutoka Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo hawataruhusiwa kuingia nchini Uingereza na katika matai [ ... ]

KIJANA WA MIAKA 20 AMTEKA NYARA BABA YAKE NA KUDAI ALIPWE FIDIA.
21 Jan 2021 16:09 - Grace Melleor

Polisi wamemkamata mwanamume mmoja aliyejulikana kwa jina la Abubakar Amodu mwenye umri wa miaka 20, ambaye alipanga nja [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2021 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.