Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.
Watu zaidi ya Milioni 13 sasa wameambukizwa virusi vya Corona duniani, wakati huu Shirika la Afya Duniani, WHO, likiendeleaGG kusema hali inaendelea kuwa mbaya.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani, nchi ya Marekani inaongoza kwa maambukizi zaidi ya Milioni tatu, ikifutwa na Brazil, India, Urusi na Peru.
Marekani imeshuhudia ongezeko la maambukizi wakati kukiwa na mvutano kati ya wataalamu wa afya na Rais Donald Trump.
Marekani imerekodi vifo zaidi ya 135,000 kwa mujibu wa Chuo cha Johns Hopkins.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anaonya kuwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi iwapo mataifa mbalimbali duniani hayatachukua hatua zaidi za kukabiliana na virusi hivyo.
Shirika hilo la Afya Duniani linaeleza kuwa janga la corona linaweza kuwa "baya na baya zaidi'' ikiwa serikali zitashindwa kuchukua hatua madhubuti.