Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Noah ambayo ilikuwa ikitokea Morogoro kwenda Dodoma na kugongana na Lori.
Kamanda Muroto amesema katika ajali hiyo watu watano wamefariki Dunia huku wengine wawili wakijeruhiwa.
Aidha, Kamanda Muroto ametaja chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa dereva wa Lori ambapo aliingia katika barabara kuu bila kuangalia pande zote za barabara akitokea kituo cha mafuta na kusababisha gari hiyo ndogo aina ya Noah kuingia kwenye uvungu wa Lori na dereva wa Lori ametoroka huku jeshi la polisi linaendelea kumtafuta.