Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeruhusu kuanzia leo safari za ndege za kitalii kuwasili nchini baada ya mambukizi ya virusi vya Corona kupungua.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmood Thabit Kombo amesema serikali imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na kiasi kidogo cha maambukizi ya corona.
Aidha,Waziri Kombo ameeleza pamoja na serikali kuruhusu shughuli za utalii kuendelea ni vyema shughuli hizo zikaendeshwa kwa kuzingatia tahadhari ya virusi vya corona kwa wageni kupimwa kila wanapoingia nchini.