Star Tv

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amezindua kituo cha huduma za simu kwa wateja.

Kituo hicho ambacho kimezinduliwa leo kazi yake kubwa itakuwa ni kutoa elimu sahihi kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya Afya yakiwemo magonjwa ya milipuko.

Kituo hicho kina uwezo wa kupokea simu 1000 kwa watu mmoja na kuunganisha vituo vitano kwa wakati mmoja.

Waziri Ummy ameelezea kazi ya kituo hicho kuwa ni kupokea maoni, taarifa, maswali na ushauri kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya afya na amewataka wananchi kupiga simu 199 ili wapate huduma hiyo na walioko nje ya nchi wanapaswa kupiga namba.0800110124.

Katika uzinduzi huo Waziri Ummy ametoa rai kwa watakaopiga simu kuwa wastaarabu, kutumia lugha ya staha, na kutoa taarifa sahihi ambazo zitaisaidia serikali na Wizara ya Afya kuchukua hatua stahiki na kwa wakati.

Kituo hicho kilichozinduliwa leo kitakuwa na wataalamu 150 wakiwemo wa afya, Wauguzi na Madaktari.

Amependekeza kituo hicho kipewe jina la “Afya Call Centre’ badala ya jina la “Kituo cha Huduma za Simu” ambacho kitakuwa kikishughulikia magonjwa yote.

Waziri Ummy amesema endapo Wizara ya Afya itaweza kutumia vizuri Tehama, itatatua changamoto mbalimbali zilizoko kwenye Sekta hiyo, Huku akiitaka Jamii itambue kinga ni bora kuliko tiba.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.