Star Tv

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan amefariki Duni leo saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan iliyopo Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Marehemu Jaji Ramadhan aliwahi kutumikia nafasi mbalimbali na kupata vyeo vya juu katika serikali ya Tanzania ikiwemo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Visiwani mwaka 2002 hadi 2007, pia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar katika kipindi hichohicho.

Pia alishakuwa Brigedia Jenerali ambapo aliwahi kulitumikia Jeshi, na hadi anafariki alikuwa ni Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar, na Jaji Mstaafu Ramdhani aliwahi kuwa Jaji Mkuu Zanzibar.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.