Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee wa Chama cha ACT Wazalendo Wilson Mushumbusi ameiomba Serikali kuunda Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itakayosimamia uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuzingatia misingi ya haki na demokrasia.
Taarifa na Rachel Dickson.
Hayo yamejiri wakati akihutubia mkutano wa kuchagua mwenyekiti wa ngome ya wazee wa chama cha ACT Wazalendo jijini Dar es salaamWilson Mushumbusi amesema tume huru itasaidia kuondoa ubaguzi wa wazee kwa misingi ya milengo ya vyama vya siasa.
Kwa upande wake Mwenyikiti wa Taasisi Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema uchaguzi huo Ngome ya Wazee wa chama cha ACT Wazalendo utaleta mabadiliko katika kuwasimamia wazee hasa katika chama kwa usawa na haki.
Uchaguzi wa ngome ya wazee wa Chama cha ACT Wazalendo ni wa tatu ndani ya chama hiyo ukitanguliwa na ule wa wanawake na vijana huku ikiwa imebakia wa kumchagua kiongozi wa mkuu wa chama ambao unatarajia kufanyika hivi karibuni.
Mwisho.