Star Tv

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Happiness Israel anadaiwa kupigwa risasi ya paja na mpenzi wake Salum Athman chanzo kikiwa bado hakijajulikana.

Tukio hilo limetokea katika Hoteli ya Kilimanjaro Mtaa wa Nyamalembo Mjini Geita ambapo wapenzi hao walichukua chumba na kukaa hapo kwa siku mbili.

Taarifa na Salma Mrisho.

Happiness na Salum ni wafanyabiashara ambao wote ni wakazi wa Mwanza wamekua katika mahusiano kwa miaka 11 na ndani ya miaka mitant mahusiano yao yalisimama lakini kufika Geita na kukaka pamoja haijajulikana kama walikua wanajaribu kurudiana katika mahusiano yao au kuyasitisha.

Wafanyakazi wa Kilimanjaro wanasema wakiwa katika shughuli zao walisikia kelele na mmoja wa wafanyakazi hao akaenda kuangalia kujua kulikoni na kukuta mtuhumiwa amembeba Happiness huku damu zikimwagika ndipo alipopiga kelele na kisha Salum akamnyoshea bastola na kisha mhudumu huyo akaanguka.

Baada ya tukio hilo Happiness aliwahishwa Hospitali ya Teule ya Mkoa wa Geita ambapo Dakatri Shabani Masawe amesema majeruhi amejeruhiwa kwa risasi eneo la kwenye paja karibu na goti.

Halikadhalika tukio hilo limesababisha majeruhi mmoja aliyejulikana kwa jina la John Christian mfanyakazi wa Kilimanjaro Hotel akiwa na michubuko maeneo mbalimbali ya mwili wake ambapo anaendelea na matibabu Hospitalini hapo.

Mtuhumiwa Salum Athmani anashikiliwa na jeshi la polisi huku upelelezi unaendelea ili kujua dhamira ya tukio hasa kwa Salum kumjeruhi mpenzi wake kwa kiwango hicho ilikua ni nini.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema kwa upande wa mtuhumiwa bado hawajafahamu lengo lake lilikuwa ni nini mpaka kumpiga risasi mpenzi wake na bado sasa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi.

                                             Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.