Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania TEC Padre Dokta Charles Kitima amesema kipindi cha kwaresima ni fursa ya kujitafakari na kumpa Mungu nafasi ya kwanza katika maisha pamoja na kutambua nafasi ya Mwenyezi Mungu kwa maisha ya kila siku kwa wakristo na wasio wakristo.
Taarifa na Piensia Rugarabamu
Padre Dokta Charles Kitima ametoa kauli hiyo wakati wakristo wakielekea katika mwezi wa toba ambapo amewataka waumini kote nchini kutambua nafasi ya muumba katika maisha yao pamoja na kubadilisha mahusiano yao mabaya na Mwenyezi Mungu.
Kwa upande wake Padre Hesco Msaga amesema kipindi cha kwaresma ni safari ya kiroho ambayo kila mkatoliki anatakiwa kutafakari na kujiandaa nafsi yake na kujiweka tayari katika kipindi hiki cha toba
Katika hatua nyingine Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli wameshiriki ibada ya jumatano ya majivu katika kanisa la mtakatifu petro jijini Dar es salaam.
Mwisho.