Star Tv

Wataalamu wa afya ya Mifugo waliopewa dhamana na serikali wametakiwa kusimamia misingi ya kisheria na kuweka pembeni imani zao ili kuepuka ubaguzi wakati wa kutoa huduma kwa wafugaji.

Taarifa na Omary Hussein-MOROGORO

Wataalamu hao wamepewa onyo hilo ikiwa ni pamoja na Tanzania kuwa na zaidi ya Nguruwe Milion 2 bado hakuna ufuatiliaji wa karibu, huku wafugaji wake wakiona kama wametelekezwa.

Katika mkutano uliowakutanisha wa wanachama wa Jumuiya ya wafugaji wa Nguruwe Tanzania TAPIFA na viongozi mbalimbali wa serikali walio chini ya sekta ya mifugo na uvuvi mkutano huo ambao umelenga kujadili changamoto na mafanikio katika sekta ya ufugaji wa Nguruwe

Changamoto iliyopo ambayo imeelezwa ni vita ya waziwazi kuonekana kuwa shughuli za ufugaji wa nguruwe si jambo la kawaida, hali ambayo imeonekana kwa baadhi ya wataalam wenye dhamana serikalini wamekosa usawa katika uendelezaji wa sekta hiyo muhimu.

Kilio cha wafugaji wa nguruwe ni kusimamiwa kwa sheria, kuwawezesha ufugaji wa Nguruwe kutambulika, pamoja na wanufaika kupata huduma kwa uwazi katika maeneo rafiki.

Kaimu mkurugenzi msaidizi wa mazao ya Mifugo, usalama wa chakula na Lishe kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi Gabriel Bura, amesema sheria ipo wazi ambayo imebainisha wajibu wa watumishi kuwa hakuna ubaguzi katika utoaji wa huduma za mifugo.

Afisa Usajili kutoka Bodi ya Nyama Tanzania Ezekiel Maro, amesema kwa hatua iliyofikiwa mpaka sasa ingetegemewa kuwepo maeneo maalum ya biashara hiyo ikiwemo Bucha na machinjio kwa ajili ya nguruwe.

Aidha, kutokana na kasi ya ukuaji wa uchumi imeelezwa huenda Tanzania ikakabiliwa na upungufu wa zaidi ya tani laki mbili za nyama nyekundu ifikapo mwaka 2022, na ili kukabiliana na upungufu huo mkakati ni kuongeza uzalishaji wa nyama nyeupe yakutosha, ambapo ufugaji wa kuku pamoja na nguruwe vikielezwa kuwa vinapaswa kupewa kipaumbele.

                                       Mwisho.

 

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.