Star Tv

 

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amekutwa na kesi ya kujibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kuyatenda Oktoba 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Hayo yamejiri siku moja tu baada yakiongozi huyo kurejea nchini baada ya kumaliza ziara yake katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani na Uingereza.

Ziara hiyo ambayo ilizua gumzo hapa nchini  hususani baada ya Zitto kubainisha wazi kuiandikia barua Benki ya Dunia kusitisha mkopo wa elimu kwa Tanzania.

Baadhi ya wanansiasa kutoka Chama tawala walitoa kauli za kutishia uhai wa mwanasiasa huyo huku yeye mwenyewe akidai kuwa kumekuwa na mipango ya "kumbambikia kesi ya uhujumu uchumi."

Mahakama ya Kisutu chini ya hakimu mwandamizi Huruma Shaidi imemkuta mwanasiasa huyo na kesi ya kujibu leo Jumanne Februari 18.

Zitto sasa anatarajiwa kujitetea kwa siku nne mfululizo mwezi ujao kutoka Machi 17 mpaka 20 ambapo mashahidi 10 wanatarajiwa kumtetea kiongozi huyo kwenye kesi hiyo inayomkabili.

Aidha, kesi hiyo itaanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Machi 17, 18, 19 na 20, mwaka huu.

Mashtaka ya Zitto yanatokana na kauli zake za kulitaka jeshi la polisi kutolea maelezo kile alichokiita mauaji ya polisi na raia yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.

                                                                      Mwisho.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.