Star Tv

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohamed Shein amesisitiza umuhimu wa kutazama upya sheria zinazosimamia mwenendo wa usalama wa chakula nchini ili kuondoa malalamiko ya wafanyabiashara.

Dk. Shein ametowa ufafanuzi huo, wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi ya Wizara ya Afya, kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba, 2019, hafla iliyofanyika Ikulu mjini hapa.

Amesema kuna umuhimu kwa Uongozi wa Wizara hiyo kuziangalia upya sheria zinazosimamia usalama wa chakula, hususan katika suala zima la ukaguzi wa bidhaa zinazotoka na kuingia nchini.

Amesema Serikali haiwezi kupuuza malalamiko ya wafanyabiashara hao na kubainisha kuwa itafanya juhudi za kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili kuondokana na  malalamiko.

Ameushauri uongozi wa Wizara hiyo kuendleea kuviimarisha vituo vya Afya , hususan vile vilioko vijijini kisiwani Pemba kwa kuvipatia nyenzo, vifaa tiba na dawa.

Aidha, ameipongeza Wizara hiyo kwa juhudi kubwa inazoendelea kuchukuwa katika kukabiliana na ugonjwa wa malaria, sambamba na kupunguza kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka asilimia 0.6 hadi kufikia asilimia 0.4.

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ameutaka uongozi huo kufanya juhudi kukiimarisha kitengo cha mifupa katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja.

Mapema, Waziri wa Wizara Afya Hamad Rashid Mohamed akiwasilisha muhtasari wa utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara hiyo, alisema katika kipindi hicho Wizara ilipanga kutumia zaidi ya shilingi

Mshauri wa Waziri katika Wizara hiyo, Mohamed Saleh Jidawi, alipongeza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, chini ya uongozi wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein katika kuimarisha huduma za afya nchini.

                                                                                                  Mwisho

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.