Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Emmanuel John mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Mori wilayani Rorya mkoani mara amepoteza maisha kwa kusombwa na maji katika mto Mori wakati akijaribu kuvuka kuelekea kijini kwake ambapo kijiji hicho kinatenganishwa na mto huo.
Taarifa na Jumanne Ntono
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mori Nyamuhanga Chacha amethibitisha tukio hilo na kueleza kwamba marehemu Emmanuel John alizama mnamo tarehe saba februari mwaka huu wakati akijaribu kuvuka mto huo kuelekea nyumbani kwake katika kijiji cha mori
Wakazi wa vijiji vya Mori na Randa wamesema kwamba kukosekana kwa daraja katika eneo hilo la mto Mori kumesabisha watu kadhaa wa vijiji hivyo kupoteza maisha
VIjana zaidi ya 40 waliojitolea kutafuta mwili wa marehemu ambaye alipatikana baada ya siku tano toka azame wameeleza kwamba ukosefu wa vifaa sahihi vya kutumia wakati wa zoezi hilo vimesababisha kuchelewa kupata mwili wa marehemu.
Marehemu Emmanuel John ambaye alipatikana amepoteza maisha ndani ya mto Mori ameacha wajane wawili na watoto wawili,
Mwisho .