Serikali inaendelea kuchunguza kwa kina uwepo wa tishio la uvamizi wa Nzige ambao wanadaiwa kuingia katika maeneo ya Mwanga na Holili mkoani Kilimanjaro mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Taarifa na Zephania Renatus
Taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na ambazo zimezua taharuki kwa watanzania ni juu ya tishio la uvamizi wa Nzige ambao wanadaiwa kuingia katika badhi ya maeneo ya Wilaya ya Mwanga karibu na nchi jirani ya Kenya.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mghwira amezungumza na waandishi wa habari na na kuwatoa wasiwasi watanzania kuwa nzige hao huenda walipita tu katika baadhi ya maeneo ya Mkoa huo.
Taarifa hiyo inakuja huku baadhi ya wakazi wa maeneo ya Holili na Taveta katika Mpaka wa Tanzania na Kenya hawajaona nzige hao na bado wanaonekana katika baadhi ya maeneo ya nchi jirani ya Kenya.
Wakati hofu hiyo ikiendelea kutanda ,hata hivyo wakulima katika maeneo ya mpakan wanaomba serikali kuchukua tahadhari kabla wadudu hao hawaingia nchini Tanzania.
Mwisho