Star Tv

Bingwa wa Dunia wa Mchezo wa Karate Rutashobya Rwezahula  amesema Tanzania inaweza kutoa Mabingwa wengi katika Mchezo huo endapo Serikali itauingiza  Mchezo huo katika Mtaala wa Elimu ili Ufundishwe Mashuleni.

 

Wanasanaa za Mapigano kundi la Jet kan du kungfuu la Jijini Arusha wanapata Mafunzo kutoka kwa Mkongwe wa Mchezo huo Sensei Wille Ringoo aliyeambatana na Bingwa wa Dunia wa Karatea mwaka 2014 Rutashobya Rwezahula.

 

Bingwa huyo wa Dunia amesema kwa Sasa sanaa hiyo inakuwa na ili ikue zaidi nakutoa Wachezaji hodari wenye sifa za Kimataifa kuna haja ya kuwekeza kwa Chipukizi ikiwemo serikali kuruhusu Mchezo huo ufundishwe Mashuleni.

 

 Mkongwe wa Mchezo huo Sensei Wille Ringo  anawataka wanasanaa hao kuzingatia suala la nidhamu litakaloondoa fikra potofu kwa jamii juu ya Mchezo huo.

 

Uongozi wa Jet kan duu Kung fuu Ngazi ya Taifa umesema tayari wameanza mikakati ya kuutangaza Mchezo huo katika Mikoa Mbalimbali ikiwemo kutumia wakongwe kutoa Mafunzo.

 

Zaidi ya Wana Jet Kan Do Kung fuu 50 Kutoka Jijini Arusha wamepata Mafunzo ya Awali Juu ya Mbinu mbalimbali za kujihami na zile za Mashindano.

 

Mwisho.

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.