Star Tv

Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa amesema taifa haliwezi kupiga hatua kiuchumi endapo sekta ya maji haitopewa mkazo kwa kuwa sekta hiyo ndiyo inaunganisha sekta zote muhimu na ametoa wito kwa wadau wa maji kuhakikisha wanalinda vyanzo vya maji ili kuendana na kasi ya sasa ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Taarifa na Adam Damian

Waziri Mbarawa amebainisha hayo katika jukwaa maalum lililokutanisha wadau wa maji  lenye lengo la kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kulinda vyanzo vya maji ili kusaidia kuwa na maji ya kutosha wakati taifa likitekeleza miradi mikubwa itakayosisimua uchumi wa taifa

Prof Mbarawa amewataka wadau kubadili mitazamo yao juu ya kulinda vyanzo vya maji nakwamba athari za uharibifu wa vyanzo vya maji nikubwa ikiwa nipamoja na kupungua kwa uzalishaji na kudidimia kwa uchumi pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Baadhi ya washiriki kwenye mkutano wa jukwaa la wadau wa maji akiwemo Katibu mkuu mstaafu wizara ya maji Mhandisi Mbogo Futakamba wameeleza namna vyanzo vya maji vinapaswa kulindwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji sambamba na kutoa elimu ya kulinda vyanzo hivyo

Katika hatua nyinge imesisitizwa kuwa ili kulinda vyanzo vya maji miti na mimea iliyokaribu na vyanzo vya maji isikatwe na kwamba shughuli zote za kibinadamu  zifanyike ndani ya mita 60 kutoka kwenye kingo za vyanzo vya maji.

                                                                                                  Mwisho

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.