Star Tv

Tanzania imesema itaiunga mkono Kenya katika nafasi ya Kiti na Mjumbe asiye wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 ikiwa ni sehemu ya ushirikiano katika masuala mbalimbali baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John alikabidhi ujumbe unaohusu kuiunga mkono Kenya kuanzia 2021/2022 ambapo Prof. Kabudi alikabidhi ujumbe unaohusu uhusiano wa Kenya na Tanzania kwa Rais Uhuru Kenyata.

Prof. Kabudi alipata fursa ya kushiriki katika uzinduzi wa ripoti ya mpango wa kujenga umoja na mshikamano baina ya wakenya ujulikanao kama Building Bridge Initiative, ambapo amewataka wakenya kushikamana na kuziba mianya ya siasa za kikabila ili kuwa na Taifa moja kwa ajili ya maendeleo.

Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta kwa upande wake amesema Taifa hilo kwa miaka mingi limekuwa likiendeshwa wa siasa za kikabila jambo ambalo amesema halileti afya kwa ustawi wa Kenya kutokana na kuwa kila baada ya uchaguzi Taifa hilo huanza kutibu majeraha yaliyotokana na uchaguzi badala ya kuzingatia masuala ya maendeleo.

Prof. Kabudi amewasilisha ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe Uhuru Kenyatta juu ya masuala mbalimbali ya mashirikiano baina ya Nchi hizo mbili na Kimataifa.

 

                                                                                 Mwisho.

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.