Star Tv

Wakazi wa kijiji cha Kitanda wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wamekumbwa na hofu ya kupata magonjwa ya tumbo kutokana na kunywa maji machafu yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu.

 Kutokana na ukame wa maji uliopo kijijini hapo, wananchi na mifugo wanategemea kisima kimoja kupata maji ya kunywa jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Wakazi hao wamesema adha ya upatikanaji wa maji inakwamisha shughuli ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba bora kutokana na umbali wanakochota maji.

 Diwani wa kata ya Likuyu sekamaganga Kasimu Gunda amesema maji hayo hayafai lakini kutokana na shida waliyonayo wananchi wanalazimika kutumia.

 Kwa zaidi ya miaka 50 wananchi zaidi ya elfu tatu wa kijji cha Likuyu Seka wanaishi kwa maji ya kisima,mwaka 2012 serikali ilipeleka mradi wa maji ili kuwaondolea kero wananchi lakini ulisimama kwa zaidi ya miaka saba, serikali ya awamu ya tano imepeleka zaidi ya shilingi bilioni nne kuuendeleza ambapo hadi sasa upo katika hatua za mwisho.

 

                                                                      Mwisho

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.