Jamii za makabila yanayojihusisha na vitendo vya ukeketaji mkoani Manyara zimesema ili ziondokane na mila hiyo ni vema zikapewa elimu kwa njia mbalimbali itakayosaidia kubadili fikra kuwa, vitendo hivyo vinafaida kwa mwanamke.
Wanajamii hao wamesema wanapaswa kupewa elimu ya kina kwa njia mbalimbali zitakazowabadilisha fikra ili kuachana na mila hiyo potofu.Baadhi ya makabila yanayojihusisha na ukeketaji mkoani Manyara ni wamasai, wairaq,wanyaturu au watatoga na wabarbaig.
Kwa upande wao viongozi wa madhehebu ya dini wanaopinga ukeketaji huo wanaona ukatili huu kwa mwanamke haufai hivyo ni vyema sheria za haki za binadamu zikasimamiwa ipasavyo.
Shirika la CSP linalojihusihsa na shughuli za kupinga ukatili kwa jamii limeanza harakati za kutokomeza vitendo hivyo mkoani Manyara kwa njia mbalimbali ikiwemo kuwaelimisha vijana wadogo.
Takwimu za mwaka 2016 zinaonyesha kuwa, mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji kwa asilimia 58.8, ukifuatiwa na mkoa wa Dodoma asilimia 47, mkoa wa Tatu ni Arusha asilimia 41,Mara asilimia 32,Singida asilimia 31 Tanga asilimia 14 na Kilimanjaro asilimia 10.
Mwisho.