Wakati Jumuiya ya Afrika mashariki inaadhimisha miaka ishirini tangu kuanzishwa kwake. inaelezwa nusu ya wakazi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo bado ni maskini wanaoishi kwa kutegemea misaada kutoka nje .
Pamoja na hali hiyo, inaelezwa kuwa kuna mafanikio yaliyopatikana miongoni mwa nchi wanachama, ingawa jitihada zinahitajika zaidi katika kuboresha hali ya uchumi wa nchi moja moja, kama anavyoeleza Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Liberart Mfumukeko.
Miongoni mwa mafanikio yanayotajwa, ni pamoja na matumizi ya lugha ya Kiswahili, licha ya kuwepo kwa mkanganyiko iwapo lugha hiyo iwe rasmi ndani ya Jumuiya au la.
Pamoja na changamoto za hapa na pale zinazoikabili jumiya hiyo, likiwemo suala la ulipaji wa ada za kila mwaka kwa nchi wanachama, sekretarieti ya jumuiya hiyo inajivunia mafanikio yaliyopatiakan hadi sasa. Injinia Steven Mlote ni Naibu katibu mkuu wa Jumuiya hiyo.
Kilele cha maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrikla mashariki, itakuwa Novemba 30 mwaka huu.
Mwisho