Star Tv

Mkoa wa Simiyu umezindua mkakakati wa kuboresha taaluma kwa mwaka 2020 ili kuinua taaluma katika maeneo yote.

Afisa Elimu Mkoa wa Simiyu, Ernest Hinju, amesema mkakati huo wa kitaaluma kwa mwaka 2020, unawaelekeza viongozi hasa wa sekta ya elimu kutumia uwezo wao kufikiri, kubuni na kuhakikisha mikakati waliyojiwekea inafanikiwa.

Akizindua mkakati huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, amesema walimu wanayo kazi moja tu ya kutibu adui ujinga, na kwamba maadui wengine ambao ni maradhi na umasikini yatatoweka wapo watu wataelimika.

Pamoja na maafisa elimu wilaya na kata, watekelezaji wakuu wa mpango huu ni walimu wakuu na wakuu wa shule ambao licha ya changamoto zilizopo wameahidi mafanikio.

Mkakati huo pia unalenga kushirikisha kada zote, ikiwemo viongozi wa kisiasa na jamii ili kufikia mafanikio ya kitaaluma.

                                                                     Mwisho

Latest News


Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.