Kila tarehe 14/10 Tanzania inaazimisha kumbukumbu ya kifo cha hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa rais wa kwanza wa Tanganyika ambaye aliaga dunia mnamo mwaka 1999.
Hii leo Hayati baba wa Taifa akitimiza miaka 20 tangu kutokea kwa kifo chake. Maadhimisho ya muasisi wa Taifa la Tanzania yamefanyikia Kitaifa mkoani Lindi. Hayati Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, Mkoani Mara, nchini Tanzania.
Hayati Nyerere anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu. Pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika barani kote hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.