Watu wenye Ualbino mkoani Mara wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa mafuta maalumu wanayotumia kupakaa ngozi zao ili kuepusha vidonda na michubuko ya ngozi inayosababishwa na mionzi ya jua hali inayopelekea baadhi yao kukumbwa na magongwa ya saratani ya ngozi.
Mionzi ya jua ni changamoto kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albinizim) ,kutokana na hali hiyo mafuta maalumu kwa ajili ya kupakaa ngozi zao ndio suruhisho la changamoto hiyo,ambapo watu hasa wanaoishi maeneo ya ijijini wanahitaji msaada huo ili kuepuka kukabiliwa na magonjwa ya saratani ya ngozi , mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Tawi la Tarime Joseph Sinda amekiri kuwepo changamoto ya ukosefu wa mafuta hayo licha ya kuwepo kwa serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia . Pia Chama cha watu wenye ualbino wilaya Tarime kimetoa shukrani kwa serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kuwaamini na kuwateua watu wenye ualbino katika nafasi mbalimbali za uongozi ambapo wameomba jamii nayo kuwapa ushirikiano. Sinda ameiomba jamii kuacha kuwaamini waganga wa kienyeji wanaowaaminisha kwamba viungo vya mtu mwenye ualbino vinaleta utajiri.