Star Tv

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Nzega Mkoani Tabora imemuagiza injinia wa Mamlaka ya Barabara mijini na vijijini Tarula kumsimamisha kazi na kukatisha mkataba wa Ujenzi kampuni ya Didia Inayojenga Daraja la Mto Nhobola baada ya kushindwa kazi.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupulla amesema mkandarasi huyo ameshindwa kufanya kazi kutokana na mkataba kumtaka kuanzi kazi mwezi Januari 2019 na kumaliza Julai 2019 lakini hakuna kazi yoyote iliyofanyika.

Ameongoza, Daraja hilo ni miongoni mwa ahadi za Mh,Rais Dk;John Pombe Magufuli dhidi ya wananchi wa Kijiji cha Nhobola ambao wamekuwa wakipata adha ya kuvuka nyakati za mvua za masika hali ambayo hugeuka kijiji hicho kuwa kisiwa.

Amemuagiza Injinia wa Tarula mkoa wa Tabora Regnard Silanga kumtoa mkandarasi huyo kisha kutangaza tenda ili apatikane mkandarasi mwingine atakayeweza kujenga Daraja hilo kwa muda uliopangwa.Daraja hilo lilitengewa shilingi milioni 440 za ujenzi pamoja na kukarabati barabara ili wananchi hao wafanye shughuli zao za maendeleo pamoja na kuondokana na usumbufu. Mkandarasi huyo tayari amesimamishwa na mchakato wa kumpata mkandarasi mwingine unaendelea ili akamilishe ujenzi huo ambao ni hitaji la wananchi.

Latest News

WATU WATANO WAFARIKI BAADA 'KUSHIKWA MATEKA' KANISANI.
11 Jul 2020 16:57 - Grace Melleor

Watu watano wameuawa baada ya washambuliaji kuvamia kanisa moja Afrika Kusini wakati malumbano yanaendelea juu ya uongoz [ ... ]

RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA KUWA MGOMBEA MWENZA.
11 Jul 2020 16:21 - Grace Melleor

Rais Magufuli amemchagua Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea mweza katika Uchaguzi wa Urais wa Tanzania, Oktoba 2020.

TANZANIA, CHINA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO.
10 Jul 2020 13:10 - Grace Melleor

Tanzania na China zimeahidi kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na maendeleo  [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.