Star Tv

Siku chache baada ya Rais, Dk; John Magufuli kutangaza Msimamo wa kusitisha ujenzi wa Mradi mkubwa wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani, mkuu wa wilaya hiyo Bi.Zainabu Kawawa amewataka wananchi kukumbuka kuwa, Wilaya yao ndio ilikua makao makuu ya wakoloni na masharti yaliyowekwa na wawekezaji waliokuwa wanatekeleza Mradi huo ni zaidi ya unyonyaji uliofanywa na wakoloni waliotawala miaka hiyo kabla ya Uhuru.

Miongoni mwa masharti yaliyowekwa na wawekezaji ni kutaka kumilikishwa Eneo la Mradi kwa Miaka 99, Serikali kutochukua kodi yoyote kwa kipindi hicho, Nchi kugharamia utekelezaji wake sambamba na kutoendelezwa kwa bandari nyingine yoyote.

Msimamo huo wa mkuu wa wilaya unakuja akisema dhamira yake ni kutekeleza na kusisitiza Msimamo wa Rais , uliotokana na masharti yaliyo onekana kuwa kandamizi kwa jamii yake, na kupelekea mradi huo kuonekana hauna manufaa yoyote kwa Taifa. Anasema kilicho msukuma Mhe. Rais John Pombe Magufuli kufanya maamuzi hayo magumu,  ni kulenga kutetea maslahi mapana ya Nchi wakiwemo wakazi wa Bagamoyo,  kulikolengwa kutekelezwa Mradi huo, kwakua masharti ya wawekezaji hayana manufaa yoyote kwa taifa. 

Anasonga mbele zaidi kwa kuwataka wakazi wa Bagamoyo kuendelea kuwa na subra, sambamba na kutanguliza imani na serikali,  kwani dhamira ni kuhakikisha Rasilimali zilizopo nchini zinatumika kwa manufaa ya Nchi,  na si kwa wawekezaji pekee. Nao wakazi wa Bagamoyo kulikolengwa kutekelezwa mradi huo wanasema walitegemea kunufaika na uwepo wa Bandari kwa kutambua umuhimu wake,  lakini baada ya kusikia masharti ya wawekezaji toka kwa viongozi wanaona , wanaona hatua za kusitisha ni kunusuru kupoteza haki ya kunufaika na Rasilimali zao. Hivi karibuni akiwa katika kikao na wafanyabiashara Rais Magufuli aliweka wazi msimamo wake wa kusitisha kutekeleza Mradi huo akisema haoni faida kutokana na masharti ya wawekezaji. Msisitizo wa mkuu wa wilaya Bi.Zainabu Kawawa ni kuwataka wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi wao wakati jitihada zikiendelea kutetea maslahi ya taifa katika matumizi ya Rasilimali.

 

 

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.