MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyongwa hadi kufa watu Watatu   kwa kuhusika na mauaji ya wakazi  wanne wa kata ya Katoma  wilaya ya Bukoba  Mkoani Kagera  mwaka 2015.

Washtakiwa hao Watatu Aliyuu Dauda ,Rashid Athuman  na Ngesela Keya  wametiwa hatiani baada ya kuhusishwa na Mauaji ya mfululizo yaliyokuwa yakitokea kuanzia mwezi  Januari hadi Novemba  mwaka 2015  maarufu kama  mauaji ya Makoromeo kutokana na watu waliokuwa wakikutwa wameuawa

Washtakiwa katika kesi hiyo namba  66 ya mwaka 2017 wamedaiwa kutekeleza mauaji ya Marehemu Vedasto John  ,Anastella Paschal  ,Emmanuel Joseph  na Evodius Aloys kwa siku tofauti  katika mwezi Oktoba  Mwaka 2015 katika kata ya Katoma wilaya ya Bukoba  Vijijini.

Jaji Mfawidhi  Lameck Mlacha   akisoma hukumu hiyo amesema hukumu hiyo  imezingatia ushahidi wa kimazingira,kukiri pamoja na baadhi ya vitu walivyokutwa navyo washtakiwa  ambavyo vilitumika kutekeleza mauaji hayo.

Akisoma hukumu iliyochukua takribani saa mbili na nusu Jaji Mlacha  amesema  hakuna ushahidi unaoonyesha watuhumiwa hao wakitekeleza mauaji  hayo moja kwa moja lakini ushahidi wa kimazingira umebaini kuwepo kwa mawasiliano ya karibu ya washtakiwa wote Watatu .

Aidha Jaji Mlacha amesema mkanda wa CD umeonyesha washtakiwa hao wakikiri mbele ya viongozi wa eneo husika  na polisi kuwa walidhamiria kufanya mauaji hayo kutokana na imani za kidini huku vipimo vya DNA vikionyesha kuwepo na uhusiano  kati ya sime na mapanga vilivyotumika katika mauaji baina ya Washtakiwa  na baadhi ya sehemu za miili ya marehemu hao kama nywele na kucha. Kadhalika   namba ya  simu ya mmoja wa marehemu hao ilipatikana ikiwa imewekewa namba za  mshtakiwa wa pili ambaye ni Rashid Athuman  ambaye aliitumia kuwasiliana na washtakiwa wenzake mara kwa mara kuhusiana na mipango yao ya kutekeleza mauaji zaidi.

Aidha washtakiwa hao walikutwa wakiwa na baadhi ya nyaraka za makanisa mbalimbali Kumi  na Matatu  yaliyochomwa moto kwa   nyakati tofauti mwaka 2015. Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo umeongozwa na wakili Mkuu wa serikali  Hashim Ngole  ilhali upande wa utetezi ukiongozwa na Mathias Rweyemamu  ambaye amesema jopo lake linatarajia kuandaa hoja za kukata rufaa kwa watuhumiwa hao ambao Mnamo Mwezi April  mwaka huu walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya Kuchoma makanisa kumi na matatu  katika wilaya za Missenyi,Bukoba na Muleba

Latest News

Kiwanda cha Alizeti chakosa malighafi, Mara
17 Jul 2019 13:12 - Kisali Shombe

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imetenga zaidi ya shilingi milioni ishirini na tano ili kuwapa wakulima  [ ... ]

Mtendaji awekwa ndani kwa kula fedha za vitambulisho.
16 Jul 2019 14:01 - Kisali Shombe

Mkuu  wa  wilaya  ya  Kalambo Julieth Binyura  amemweka ndani  kwa muda  wa  saa 24 mtendaji  wa  kijiji cha  [ ... ]

Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na M...
16 Jul 2019 12:49 - Kisali Shombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 5 kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2019 k [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.