Bodi ya tumbaku nchini,TTB imetoa onyo kwa watendaji wa makampuni ya ununuzi wa tumbaku wanaokwenda kinyume na sheria kanuni na taratibu za masoko ya tumbaku.
Masoko ambayo yanayoendelea ambayo wakulima walikuwa wanayalalamikia na bodi kuchukua hatua. Wakulima wanapongeza hatua iliyofanywa na Serikali kupitia Bodi ya tumbaku. Tangu masoko yaanze karibu mwezi uliopita jumla ya kilo milioni ishirini za tumbaku kati ya kilo milioni sitini na moja ,zimenunuliwa na makampuni ya ununuzi wa tumbaku zenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni sitini.