KUKITHIRI kwa tabia ya ulevi wakupindukia kwa baadhi ya wazazi na walevi mjini Iringa, kumetajwa kuathiri kundi la watoto na kusababisha idadi kubwa ya watoto kuishi katika mazingira hatarishi, baada ya wazazi wao kutozingatia mahitaji ya familia zao.
Ulanzi ni miongoni mwa pombe za jadi zinazopatikana mkoani Iringa - pombe inayogemwa kuanzia mwezi wa pili mpaka mwezi wa tano, ingawa zipo pombe nyingine nyingi za jadi kama Komoni pombe inayopikwa kwa kutumia Mahindi na Ulezi, huku nayo pombe aina ya Msabe na Kimpumu zikipatikana kwa wingi mkoani Iringa, ambapo Mwenyekiti wa wenyeviti wa Kata
ya Ruaha-Timoth Kiongozi, anasema tatizo la ulevi wa pombe kwa baadhi ya wazazi na walezi ni kubwa. Zainabu Mgimbe ni miongoni mwa viongozi wa Kata ya Ruaha, anasema katika sensa waliyoifanya katika Kata hiyo ya Ruaha, wamebaini uwepo wa idadi kubwa ya watoto waishio katika mazingira hatarishi ambao baadhi yao ni yatima na wengine wazazi na walezi wao ni walevi. Baadhi ya watotot wanakosa malezi bora kutokana na walezi/wazazi kuwa walevi.