Star Tv

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Aprili, 2019 amezindua mradi wa njia ya umeme ya msongo wa KV 220 kutoka Makambako hadi Songea na ameweka jiwe lamsingi la ujenzi wa kituo cha mabasi na barabara za lami katika Manispaaya Songea Mkoani Ruvuma.Sherehe za uzinduzi wa mradi wa njia ya umeme zimefanyika katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme kilichopo Unangwa Mjini Songea na zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Anders Sjöberg, Mawaziri, Wabunge na viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Godfrey Zambi.


Mradi huo umehusisha ujenzi wa njia ya umeme yenye urefu wa kilometa 245, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako, ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Madaba na Songea na usambazaji wa umeme wa msongo wa kilovoti 33 zenye urefu wa kilometa 900 zilizounganishwa kwa wateja 22,700 katika Wilaya za Njombe, Ludewa, Mji wa Makambako, Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga. Ujenzi wa mradi huo umegharimu shilingi Bilioni 216 na Milioni 941, fedha ambazo zimetolewa kwa mkopo nafuu kutoka Shirika la Maendeleo la Sweden na Serikali ya Tanzania, na baada ya kukamilika kwake Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezima mitambo ya kuzalisha umeme kwa mafuta katika vituo 5 na hivyo kuokoa shilingi Bilioni 9.8 kwa mwaka. Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani amemshukuru Mhe.

Rais Magufuli kwa kutilia mkazo wa kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa mara alipoingia madarakani na kwamba hivi sasa Mkoa wa Ruvuma wenye mahitaji ya megawati 12 za umeme unapata megawati 48 zitakazowezesha uanzishaji wa viwanda na vijiji vyote kupatiwa umeme ifikapo mwaka 2012. Mhe. Kalemani amebainisha kuwa tangu Mhe. Rais Magufuli aingie madarakani idadi ya vijiji vilivyopatiwa umeme kupitia Wakala wa Umeme Vijiji (REA) imeongezeka kutoka 2,018 hadi kufikia 6,464 (sawa na ongezeko la asilimia 214).

Balozi wa Sweden hapa nchini Mhe. Andrers Sjöberg ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa uhusiano na ushirikiano mzuri na Sweden ambao umesaidia kutekelezwa kwa miradi mingi ya maji tangu miaka ya 90 na baadaye kufuatiwa na miradi ya kupeleka umeme vijijini ambako wananchi wengi wamenufaika hususani wanawake.

Kwa upande wake, Mhe. Rais Magufuli ameishukuru nchi ya Sweden kupitia SIDA kwa ufadhili wake katika mradi huo na ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo pamoja na mradi mkubwa ambao Tanzania inaujenga hivi sasa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji utasaidia kuinua uchumi kupitia viwanda na pia utasaidia kuokoa mazingira kwa kuwa wananchi watatumia umeme badala ya kuni na mkaa ambao unapatikana kwa kukata miti.

CHANZO: Ikulu Dar es Salaam.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.