Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za fedha chini ya Benki kuu ya Tanzania kuanzisha  kitengo maalum ndani ya taasisi hizo kitakachokuwa kinapokea madini ya dhahabu kama dhamana ya mkopo kwa wachimbaji wa madini ikiwa ni sambamba na kuangalia namna ya kupunguza riba ili iwe nafuu kwa wachimbaji wadogo.

 

Amezungumza haya wakati wa kufunga maonyesho ya teknolojia ya dhahabu Mjini Geita. Waziri alianza kutembelea baadhi ya mabanda yakiwemo ya kifedha na kuona namna gani wanavyotoa kipaumbele katika mikopo kwa wachimbaji wadogo.

 Katika maonyesho haya ambayo kila sekta inayohusiana na madini iliweza kutoa elimu kama banda la kliniki ya biashara na banda la waja linalosisitiza utumiaji sahihi wa kemikali za dhahabu.

 

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema dhahabu ya Geita sasa inatakiwa iakisi maisha ya Wanageita kwa kupata huduma bora na wale wote waliotumia  fedha  za jamii zinazotolewa na mgodi watachukuliwa hatua.

 

Latest News

Mauaji ya kukata makoromeo, washtakiwa wahukumiwa. Bukoba
20 Jun 2019 08:21 - Kisali Shombe

MAUAJI YA KUKATA MAKOROMEO:Washtakiwa wahukumiwa kunyongwa hadi kufa Mahakama kuu kanda ya Bukoba  imewahukumu  kunyo [ ... ]

Kudorola kwa soko la Pamba.
19 Jun 2019 12:20 - Kisali Shombe

Madiwani halmashauri ya wilaya ya bariadi mkoani Simiyu wameilalamikia serikali kuhusu zao la pamba kukosa soko la uhaki [ ... ]

Adha ya maji, Kalambo
19 Jun 2019 11:23 - Kisali Shombe

Wananchi  katika   kjiji cha  Kisungamile  kata  ya  matai   wilayani  Kalambo  mkoani  Rukwa  wameiomba   [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.