Star Tv

Waziri mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa amewata Wanajumuiya ya WANAJIOSAYANSI kuwa wa kwanza kujua kinachoendelea katika sekta zote zinazowahusu  bila kujali wanafanya kazi serikalini au Shirika Binafsi kwa maslahi mapana ya Taifa.

  

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua warsha ya wana jumuiya hiyo ambapo Sekta ya Madini, Maji na mafuta ni kati ya sekta zinazowahusu wanajioSayansi.

 

Waziri wa Madini Angellah Jasmin Kairuki akitoa ufafanuzi amesema, "sekta ya madini inafulsa kubwa ili kuongeza ufanisi na uwezo wa kiuchumi wa wanajiosayansi".

 

Kwa upande wake Dk, Elisante Mshiu katibu mkuu wa wanajiosayansi Tanzania anasema lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kuleta wanasayansi ili kujadili Sayansi ya dunia na Mifumo yake.

Katika  kuhakikisha Sekta ya madini inaleta matokeo chanya hapa nchini serikali iliifanyia marekebisho ya sheria ya madini ya mwaka 2010 ili sekta ya madini iweze kumilikiwa na wazawa kwa sehemu kubwa.

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.