Star Tv

Vyama vya siasa vya upinzani nchini vimepata pigo lingine kwa kujivua uanachama wa chama cha wananchi CUF aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya chama hicho Julius Mtatiro aliyetangaza kuhamia CCM ili kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

 

Wakati akitangaza kuihama CUF na kuhamia chama cha mapinduzi CCM, Mtatiro ametoa sababu tano ikiwemo ya Serikali kutekeleza kwa vitendo ajenda za upinzani ikiwemo kupambana na ufisadi na kukithiri kwa migogoro ya kiuongozi ndani ya CUF.

 

Akizungumzia namna Serikali inavyofanyia kazi mambo ambayo wapinzania wamekuwa wakiyapigia chapuo hasa utoaji elimu bure, ujenzi wa miundombinu ya kisasa, kudhibiti rushwa na ufisadi, amesema haoni sababu ya kuendelea kuwa upande mwingine hivyo ameamua kuhamia ccm ili kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo.

 

Mtatiro amesema kuwa, amefikia uamuzi huo baada ya kufanya tathimini juu ya mustakabali wake wa kisiasa na kuongeza kuwa, kuhamia CCM kutampa fursa ya kumshauri kwa ukaribu Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho tawala ili kuwapatia wananchi maendeleo.

 

"Nimetafakali kwa kina zaidi ya mwezi mmoja, nimepata ushauri kutoka kwa ndugu na jamaa zangu wa karibu. Lakini nimewaza pia, kuna vijana umri wangu na wameisaidia nchi hii kwa kiasi kikubwa, nikajiuliza mimi nimeifanyia nini nchi hii zaidi ya kukisaidia chama cha wananchi CUF pekee. Mimi bado kijana mwenye uwezo wa kuisaidia nchi hii, hivyo nimeangalia mustakabali wangu wa kisiasa nikaona nitafute chama mbadala ambacho kitanipa fursa ya kuendeleza dhamira yangu ya kuwatumikia Watanzania" Alisema Mtatiro.

 

Aidha, Mtatiro amebainisha kuwa, watu wasifikiri kuwa kuhamia kwake CCM amenunuliwa kwani thamani yake haiwezi kununulika kwa fedha bali yeye mwenyewe bila hata kukutana na viongozi wa ccm amefikia uamuzi huo, na akawaomba viongozi wa chama hicho wampokee ili ashirikiane na wengine kumsaidia Rais kupunguza umasikini wa watu hasa ukizingatia naye ametokea familia masikini.

 

Mtatiro ambaye pia alihudumu nafasi ya ukatibu wa wabunge wanaounda umoja wa  Ukawa wakati wa bunge la katiba amedai kumuandikia barua Katibu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad  juu ya uamuzi huo lakini hakujibiwa.

 

Julius Mtatiro, amedumu ndani ya CUF kwa miaka 10. Kuondoka kwake katika siasa za upinzani kumeongeza jeraha ndani ya vyama hivyo kufuatia mtiririko wa viongozi, madiwani, na wabunge kadhaa kuhamia CCM baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

 

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.