Star Tv

Wabunge nchini Tanzania watapimwa virusi vya HIV siku ya Alhamisi ikiwa ni mfano wa kuwa katika mstari wa wa mbele katika jitihada za kupambana na ugonjwa wa ukimwi, kwa mujibu wa gazeti la Citizen la nchini humo.

Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayohusika na masuala ya HIV, Bw Oscar Mukasa, alisema Jumanne kuwa kundi hilo litaandaa shughuli kadhaa kuunga mkono kampeni ya serikali ya nchi nzima ya kupima virusi vya HIV, wakati wa kampeni iliyozinduliwa na waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa siku ya Jumanne.

Kampeni hiyo inayofahamika kama 'Furaha Yangu' inafanywa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani la USAID, mradi ya afya wa Tugole na washikadau wengie katika sekta ya afya.

Kati ya shughuli zingine ambazo zitachukuliwa na bunge kwa mujibu wa Bw Mukasa ni pamoja na kongamano kuhusu wajibu wa viongozi katika kupambana na virusi vya ukimwi.

Pia kutakuwa na maonyesho kuhusu shughuli zinazofanywa na mashirika yasiyo ya serikali katika kupambana na virusi vya ukimwi kuanzia Ijumaa hadi Jumamosi.

Kwa hisani ya BBC.

Latest News

Nape Nnauye akutana na Mhe. Rais Magufuli, amuomba radhi.
10 Sep 2019 11:44 - Kisali Shombe

Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza [ ... ]

Mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini
09 Sep 2019 09:21 - Kisali Shombe

Maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini hapo jana walikabiliana na waporaji kwa kutumia magurunedi na risasi za mpira ka [ ... ]

Kura za siri zapigwa kubaini Majambazi na Vibaka, Tabora
09 Sep 2019 09:11 - Kisali Shombe

Wananchi wa wilaya ya Igunga na Nzega mkoani Tabora wameiunga mkono Kampeni ya Fukuafukua Majambazi na Vibaka kwa kupiga [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.