Star Tv
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, February 11, 2018 alimtembelea Mbunge Singida Mashariki Tundu Lissu anayeendelea na matibabu nchini Ubelgiji. Zitto amesema amefurahi kumwona Lissu akiwa anaendelea vizuri, na afya yake kuzidi kuimarika. Akilinganisha na hali aliyomwona nayo jijini Nairobi mwaka 2017, amekiri kuwa Mwenyezi Mungu amepitisha uwezo wake na kumponya Lissu. Zitto ametaja baadhi ya mambo ambayo amezungumza na Lissu ambayo yanahusu Tanzania na pia kuhusu suala la matibabu yake “Lissu anasikitika kuwa Bunge mpaka leo sio tu halimhudumii lakini hata stahili zake za msingi kama Mbunge hapewi. Licha ya kutibiwa kwa misaada ya wasamaria wema, lakini ana mahitaji mengine kama mwanadam na wajibu kama mzazi. Sheria ya Bunge imeweka wazi kuwa Mbunge anapokuwa ametibiwa nje ya nchi Bunge humgharamia maisha yake.” -Zitto Kabwe “Mpaka sasa ni miezi mitano imepita tangu Lissu ashambuliwe kwa risasi na hakuna taarifa yeyote kuwa mamlaka za uchunguzi zimewakamata wahusika au kuonyesha tu juhudi za kuwatafuta wahusika. Jambo hili linatoa taswira mbaya sana juu ya vyombo vyetu vya uchu

Latest News

Mgogoro wa Maji unatishia Amani Duniani, inasema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa...
21 Mar 2024 14:18 - Kisali Shombe

Siku ya Maji Duniani ambayo inafanyika tarehe 22 Machi ikiwa na kaulimbiu: 'Maji kwa Ustawi na Amani. Ambapo maji ni moj [ ... ]

Matarajio katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini, Jumanne tarehe 22/2023
21 Aug 2023 12:14 - Kisali Shombe

Mkutano huo ambao utafanyikia Johannesburg nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne, tarehe 22 Agosti 2023, unatarajiwa kuhu [ ... ]

Rais Ramaphosa Kuwa Mwenyeji wa Rais Xi Jinping wa China
21 Aug 2023 11:11 - Kisali Shombe

Rais Cyril Ramaphosa Jumanne ya tarehe 22 Agosti 2023, atakuwa mwenyeji wa Mheshimiwa Rais Xi Jinping wa China katika Zi [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2024 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.