Star Tv

Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana umeipongeza serikali kwa hatua yake ya kuziondoa kaya zaidi ya 60 zilizokuwa zimejenga katika eneo la shule hiyo ili kuimarisha usalama wa wanafunzi na mali zao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana Mwl. Lydia Eliud, amesema sehemu kubwa ya shule hiyo ilivamiwa na wakazi wa Kata ya Ng’ambo hivyo kuhatarisha maisha ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu na wizi kwenye mabweni nyakati za usiku. Mkuu wa Shule ya Tabora Wavulana Mwl. Robert Marwa ameelezea ufaulu mzuri wa mwanafuzi wake Clarence Sumbuzi aliyekuwa wa 8 kitaifa kwa masomo ya Sayansi huku Agatta Nyenga aliyekuwa wa 2 kati ya Mwanafunzi 10 wa Kitaifa kutoka Shule ya Sekondari ya Tabora Wasichana .

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwl. Queen Mlozi amewataka walimu wakuu wa shule zote za Sekondari kuhakikisha wanasimamia nidhamu za wanafunzi.

Katika kikao hiki cha kazi cha wakuu wa shule za sekondari za mkoa huu wametakiwa kuchukua hatua dhidi ya wanafunzi ambao hawana nidhamu kwenye shule zao mapema ili wasiweze kusababisha vijana wengine ambao ni wazuri nao wakaiga tabia zao.

Latest News

ZIMBABWE KUKABILIANA NA WANAOIPAKA TOPE NCHI YAO.
07 Aug 2020 16:05 - Grace Melleor

Taifa la Zimbabwe limesema lipo mbioni kupitisha sheria mpya ambayo itatoa adhabu kali kwa vyama vya kisiasa vinavyofany [ ... ]

MEMBE TAYARI AJIDHATITI KWA MAPAMBANO.
07 Aug 2020 15:35 - Grace Melleor

Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe tayari amechukua fomu ya kuwania Urais wa Jamhuri ya M [ ... ]

MWANAMFALME WA SAUDI ASHUTUMIWA KWA KUTUMA MAMLUKI CANADA.
07 Aug 2020 15:21 - Grace Melleor

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ameshutumiwa kwa kutuma mamluki nchini Canada ili kumuua aliyekuwa afisa [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2020 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.