Star Tv

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara imeshindwa kufikia lengo la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 44 na milioni 236 za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2016 - 2017.

Halmashauri ya wilaya ya Serengeti iliyopo mkoani Mara, uwenda ikashindwa kufikia malengo yake ya kuwapatia huduma bora wakazi wa wilaya hiyo kufuatia kushindwa kukusanya kiasi cha shilling billion 44,236,729,524 na kuambulia mapato ya shilling billion 3,185,575,982 sawa na asilimia 10 tu ya makusanyo yote ya ndani.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wilyani humu, viongozi wa halimashauri hiyo, wamesema kuwa upungufu huo unatokana na dosali zitokanazo na watendaji kutokusimamia vema mapato.

Wakizungumzia huduma mbali mbali viongozi hawa wanasema kuwa serikali ya awamu ya tano ipo makini kuhakikisha inawaletea maendeleo wananchi wake. Halmashauri ya wilaya ya Serengeti ni kati ya halmashauri nane zilizopo mkoani Mara,pamoja na uwepo wa hifadhi ya taifa ya Serengeti katika wilaya hii bado inakabiliwa na tatizo la kushindwa kukusanya mapato yatokanayo na tozo la huduma katika mahotel ya kitalii.

Latest News

Nape Nnauye akutana na Mhe. Rais Magufuli, amuomba radhi.
10 Sep 2019 11:44 - Kisali Shombe

Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye amekutana na kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanza [ ... ]

Mauaji ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini
09 Sep 2019 09:21 - Kisali Shombe

Maafisa wa usalama nchini Afrika Kusini hapo jana walikabiliana na waporaji kwa kutumia magurunedi na risasi za mpira ka [ ... ]

Kura za siri zapigwa kubaini Majambazi na Vibaka, Tabora
09 Sep 2019 09:11 - Kisali Shombe

Wananchi wa wilaya ya Igunga na Nzega mkoani Tabora wameiunga mkono Kampeni ya Fukuafukua Majambazi na Vibaka kwa kupiga [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.