Baadhi ya vijana wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameibua fursa ya kiuchumi ya uoteshaji miti kama njia ya kuwapatia kipato kwa kuziuzia halmashauri za mkoa huo.

Zoezi la kupanda miti linasimamiwa na mkuu wa mkoa huo Agrey Mwanry.

Georgy Peter ni kijana mwenye umri wa miaka 41 mkazi wa Nzega shuguli kubwa kwake ni uoteshaji wa miti ujuzi huu na uthubutu wa kufanya kazi hii aliupata aliupata kwa kufundishwa na kuamini iko siku atakuwa mtaalamu wa kuotesha miti.

Mafanikio ya kuliteka soko la mkoa wa Tabora ni bei kuwa nzuri na umalidadi wa kazi, lakini kazi hiyo hayupo peke yake,Kemi John ndie mkewake wote hawa wamejikita katika uoteshaji wa miti na mambo yanakwenda vizuri.

Kazi hii imekuwa na mafanikio kwa Georgy, imemuwezesha kujenga nyumba bora,kusomesha watoto lakini bado haitoshi wanaendelea kuchangia na kuhamasisha upandaji wa miti katika taasisi za serikali kwa lengo la kutunza mazingira.

Waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi nyasa mbili wanaona umuhimu wa utunzaji mazingira baada ya kupewa miche 500 za miti.

Picha na mtandao.

Latest News

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:24 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Rais wa zamani wa Misri Morsi aaga dunia mahakamani
18 Jun 2019 09:23 - Kisali Shombe

Rais wa zamani wa Misri, Mohammed Morsi amefariki dunia Jumatatu (17.06.2019) baada ya kesi yake kusikilizwa katika maha [ ... ]

Chanjo ya Surua Rubella yatolewa Singida.
18 Jun 2019 08:52 - Kisali Shombe

Zaidi ya asilimia 80 ya  watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano, wamepatiwa chanjo ya  Surua Rubella  katika ha [ ... ]

Other Articles

Social Media

Copyright © 2019 . Star Tv - Tanzania. All Rights Reserved.